
Uwezeshwaji Kupitia Muziki
SAUTI IC inakupatia elimu ya muziki, fursa za kujijengea ujuzi, na programu za kubadilishana utamaduni zinazowawezesha vijana kugundua vipaji katika sauti zao, kuendeleza ujuzi kwa vitendo, na hatimaye kubadilisha mustakabali wa Maisha yao.
Katika jitihada hizi maalum, tunatafuta kuleta athari chanya itakayodumu kwa watu binafsi, jamii, na katika sekta ya ubunifu kwa mapana yake.




Jinsi SAUTI IC Inavyotengeneza Fursa
Tunajenga madaraja ya kiutamaduni tukifungua njia kwa mustakabali wa baadaye kwa kuchanganya urithi wa Kiafrika, ubunifu wa vijana, na kutengeneza miundombinu itakayoleta mabadiliko.




Programu za Muziki kwa Vijana
Tunatengeneza programu jumuishi, zinazowalenga vijana — tukianza na mafunzo ya awali kabisa mpaka mafunzo ya ngazi za juu sana — zinazowasaidia vijana kuzipata sauti zao, kujenga ujuzi wa vitendo, na kukua kitaaluma katika muziki na sanaa.
Miundombinu na Urithi wa Kitamaduni
Tunajenga shule za muziki na vituo vya mafunzo ya ubunifu vinavyohifadhi urithi tajiri wa tamaduni za Tanzania na kutengeneza fursa za kujifunza kwa kila rika. Mradi wetu wa kwanza na kielelezo — Shule ya Muziki ya Magnificat — itakuwa mahali pa uzuri, makuzi, na umoja.
Sehemu Tunazoziangazia Zaidi
Kuanzia kwenye ujuzi hadi katika mifumo, SAUTI IC inaunganisha vipaji na fursa — sauti moja baada ya nyingine.


Elimu ya Muziki
Programu zilizopangiliwa vizuri, malezi ya kitaaluma, na mafunzo ya vitendo ili kufungua uwezo kamili vipaji vya muziki na ubunifu wa vijana.


Maendeleo ya Kitaaluma
Tunawaandaa vijana kwa kazi endelevu katika sekta ya ubunifu — kuanzia kwenye utayarishaji wa muziki hadi usimamizi wa hafla na namna ya ufundishaji.


Kuonekana Kimataifa
SAUTI IC inashiriki utamaduni wa Kitanzania katika majukwaa ya kimataifa kupitia makongamano, ushirikiano, na diplomasia ya ubunifu.
Ushirikishwaji na Ushirikiano
Tunazipandisha sauti ambazo hazijawakilishwa vya kutosha — hasa za wasichana na vipaji ambavyo havijasikika vya kutosha — wakati huo-huo tukijenga ushirikiano na imani na sekta mbalimbali.
→
→
→
→



Mwonekano wa Ndoto Yetu
Tangu njozi hadi uhalisia — kutana na watu wanaobeba dhamira ya SAUTI IC mioyoni mwao na mikononi mwao.






Hizi ndizo sauti zilizo nyuma ya Kampeni ya Athari ya SAUTI — walimu, wanafunzi, waota ndoto, viongozi. Habari zao zitaeleweka kwa uwazi zaidi wakati muziki unapoanza kupigwa.
©SAUTI Impact Campaign 2025. All rights reserved

